NBC Premier League

TATHMINI KABLA YA MCHEZO : NAMUNGO V MTIBWA SUGAR

Published on

Kama kuna kitu ambacho Namungo watakuwa wanjivunia hivi sasa basi ni namna walivyocheza vizuri sana dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wao wa mwisho walioshinda kwa bao 1-0, goli zuri la Pius Buswita na kama watachukua kama mfano wa kucheza leo dhidi ya Mtibwa Sugar basi wanaweza kupata ushindi wao wa pili mfululizo.

Tangu wapate sare dhidi ya Simba, Namungo hawakurejea tena kucheza kwa kiwango kile mpaka kwenye mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji huku wakionyesha kiwango Duni  zaidi dhidi ya Geita Gold wakinyukwa 1-0, licha ya pia kushinda 2-0 dhidi ya Ihefu  lakini hawakuwa kwenye ubora wao, ila mchezo wao wa mwisho wameonekana kurejesha makali yao.

Mtibwa Sugar kwa upande wao hali ni mbaya sana kwani tangu wapate alama 3 dhidi ya Geita Gold wakiifunga 3-1 kwenye uwanja  wa nyumbani, Manungu Complex, Mtibwa wamecheza mechi 4 bila Ushindi wala Sare.

Kipigo cha 5-0 dhidi ya Azam ndio ilikuwa mechi mbovu zaidi kwao kucheza huku wakicheza katika kiwango cha chini mno. Lakini vipigo vingine ni pamoja na 1-0 dhidi ya KMC, 2-1 dhidi ya JKT Tanzania na 2-1 dhidi ya Tabora United. Mtibwa wanaburuta mkia kwenye Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara hadi sasa wakiwa na alam 5 tu.

Leo wana kibarua kigumu dhidi ya wachimba madini wa mkoani Lindi, Namungo ambao pia wana njaa ya alama 3 leo nyumbani ili kuzidi kurejesha matuamini kwenye mipango yao waliyojiwekea msimu huu. Mtibwa wana shughuli pevu ya kufanya kwani licha ya Mkuu wa Mkoa Ndugu Malima kuwapa motisha bado Mtibwa wameonekana kuwa na ugonjwa usiojulikana.

WA KUANGALIWA :

NAMUNGO : PIUS BUSWITA ; Magoli manne(4)  kibindoni hadi hivi sasa ikiwemo goli la ushindi dhidi ya Dodoma Jiji, amekuwa kwenye kiwango bora sana hivi karibuni chini ya Kocha Denis Kitambi, anatarajiwa kuongoza mashambulizi leo dhidi ya Mtibwa Sugar na kupeleka maumivu.

MTIBWA ; LADACK CHASAMBI; Bwana mdodo ameendelea kuwa gumzo mitandaoni akihusishwa kuhama ndani ya viunga vya wakata miwa hao amekuwa muhimili mkubwa kwenye safu ya suhambuliaji akiungana veme na Mateo Anthony.

Popular Posts

Exit mobile version