LA Lakers wamefanikiwa kuingia fainali ya kwanza kabisa ya michuano mipya ya NBA IN-SEASON 2023 baada ya kuwafunga New Orleans Pelicans kwa vikapu 133-89 kwenye mchezo wa Nusu fainali usiku wa kuamkia leo.
LeBron James alikuwa nyota wa mchezo huo akifunga vikapu 30, akishinda mipira ya kurejea mara 5 na kutoa pasi za usaidizi 8 huku Anthony Davis(16), Austin Reaves(17) na DeAngelo Russel(14) wakichagiza alama nyinginezo.
Lakers watacheza na Pelicans ambao wao wamewapa kipigo cha mshituko Milwaukee Bucks cha vikapu 128-119 na kutinga hatua hiyo.
Fainali inatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi, Disemba 19 2023.