NBC Premier League

BARES AOMBA KUONDOKA MASHUJAA FC.

Published on

Miongoni mwa timu zilizokuwa zinapigiwa chapuo la kufanya vizuri baada ya kupanda daraja msimu huu ni klabu ya Mashujaa kutoka Kigoma.

Kila shabiki na mwanamichezo aliamini hakuna timu itakayoenda pale kigoma na kupata matokeo na badala yake baada ya michezo kadhaa ya Ligi hali imebadilika kila timu inayoenda pale imekuwa ikipata matokeo.

Hadi kufikia hivi sasa klabu ya Mashujaa imecheza mechi nane [8] mfululizo bila kupata ushindi katika michezo ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu ilipopanda daraja msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kuwa tayari kocha mkuu wa kikosi hicho Abdallah Baresi ameandika Barua ya kujihudhuru kuifundisha timu hiyo mara baada ya kupokea kipigi cha 2-0 kutoka kwa Tanzania Prison.

Mashujaa imecheza michezo saba [7] nyumbani,

  • Ushindi michezo miwili [2].
  • Kupoteza michezo mitatu [3].
  • Sare michezo miwili [2].
  • Imefunga magoli sita [6].
  • Imefungwa magoli tisa [9].

Mashujaa imecheza michezo minne [4] Ugenini.

  • Haijapata ushindi wa aina yoyote.
  • Imepoteza michezo mitatu [3].
  • Sare mchezo mmoja [1].
  • Imefungwa magoli sita [6].
  • Imefunga magoli mawili [2].

Jumla imecheza michezo kumi na moja [11] ya Ligi hadi hivi sasa.

  • Imeshinda michezo miwili [2].
  • Imepoteza michezo sita [6].
  • Sare michezo mitatu [3].
  • Imevuna alama tisa [9].
  • Ipo nafasi ya kumi na tano [15] ya msimamo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.

Mchezo unaofuata kwa klabu ya Mashujaa itakuwa shidi ya Mtibwa Sugar December 18 katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

Ikumbukwe Mtibwa Sugar pia ipo nafasi mbaya zaidi kwenye msimamo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ikiwa mkiani mwa msimamo wa Ligi na alama tano [5] ikiwa imecheza michezo kumi na mbili [12].

Popular Posts

Exit mobile version