Top Story

KIEMBA ATAMANI KUCHEZA NA AUCHO NA CHAMA.

Published on

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Nigeria Jay jay Okocha amesema kama angebahatika kucheza timu moja na Michael Essien pamoja na Yaya Toure basi ubora wake ungekuwa ni mara dufu ya ule ambao ailiuonesha.

Okocha aliongeza kuwa wachezaji hao [Essien na Toure] walikuwa wanatumia nguvu kukaba wakati timu haina mpira kwa hiyo pindi timu ikiwa na mpira yeye ndio angekuwa anafanya mabalaa!

Kwa upande wa Amri Kiemba, mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na klabu kadhaa nchini, amesema amepata bahati ya kucheza na wachezaji wengi bora katika wakati wao, baadhi yao ni Chuji, Boban, Kazimoto, Banka, Ngasa, Mahadhi, Chombo, Sure Boy, Samatta.

Kama ningekuwa nacheza nyakati hizi basi natamani ningecheza pamoja na Khalid Aucho na Clatous Chama halafu na mimi wa tatu! Yale ambayo nilishayafanya basi yangekuwa maradufu.

Unacheza na mchezaji anakaba kama Aucho, mimi na Chama kazi yetu inakuwa ni kwenda mbele tu kutafuta magoli.

Amri Kiemba, Mchezaji wa zamani wa Simba, Yanga na Azam FC.

Popular Posts

Exit mobile version