Serengeti Lite Women Premier League

YANGA PRINCESS MSHINDI WA TATU NGAO YA JAMII.

Published on

Klabu ya soka ya wanawake ya Yanga Princess imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ya michuano ya ngao ya jamii iliyokuwa ikiendelea katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Jijini Dar Es Salaam.

Yanga Princess imeifunga Fountain Gate Princess kwa mikwaju ya Penalty 4-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya 0-0.

Fountain Gate princess ilipoteza mchezo wa kwanza wa michuano ya ngao ya jamii kwa kipigo cha goli 5-0 kutoka kwa JKT Queens.

Yanga Princess ilipoteza kwa mikwaju ya penalty mbele ya Simba Queens katika mchezo wa kwanza wa ngao ya hisani.

Mchezo unaofuata jioni hii ni fainali ya ngao ya jamii kati ya Simba Queens dhidi ya JKT Queens pale Azam Complex, Chamazi, Dar Es Salaam.

Popular Posts

Exit mobile version