Klabu ya Yanga haijawahi kupata ushindi wowote kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika tangu Ligi hii ianzishwe.
Yanga imecheza jumla ya mechi tisa [9] imetoa sare michezo minne [4] na imepoteza michezo mitano [5], imekusanya alama nne [4] pekee.
Leo Yanga inashuka dimbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Medeama katika mwendelezo wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika hatua ya makundi ukiwa ni mchezo wa nne [4] msimu huu.
Yanga msimu huu kwenye Ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi imefunga magoli mawili [2], imeruhusu magoli matano [5], imekusanya alama mbili [2].