Manchester United imeungana na Atletico Madrid katika kupinga uanzishwaji wa michuano ya European Super League licha ya mahakama kuruhusu michuano hiyo iendelee.
Manchester United wamesema hawapo tayari kushiriki michuano hiyo na watasalia kuwekeza nguvu zao katika mashindano yaliyo chini ya shirikisho la soka Barani Ulaya [UEFA].
“Nafasi yetu haijabadilika”.
“Tunaendelea kuwekeza nguvu zetu katika ushiriki wa michuano ya UEFA, na ushirikiano imara na UEFA, Ligi kuu England na klabu zingine kupitia ECA kwaajili ya maendeleo ya michezo Ulaya”.
- Waraka wa Manchester United baada ya Mahakama ya Usuluhishi kuruhusu michuano ya European Super League kuendelea.
Klabu zingine ambazo zimetangaza kutoshiriki michuano hiyo ni PSG, Bayern Munich, Sevilla, Valencia na Villareal na klabu zote zimeandika waraka wa kutokushiriki.