Mchana huu kimetangazwa kikosi cha wachezaji 25 cha timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoingia kambini Tarehe 25 kwa ajili ya kujiandaa na Mchezo wa Kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya soka ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.
Wachezaji hao ni kama taarifa kutoka TFF inavyojieleza :
Kikosi hicho kimetokana na kikosi cha awali cha wachezaji 53 kilichotangazwa kwa ajili ya kujiandaa na AFCON.
Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kupigwa siku ya Alhamisi, Tarehe 27 ikiwa pia inaenda sambamba na uzinduzi wa uwanja wa Amaan uliokwishafanyiwa ukarabati mkubwa.