Kocha mkuu wa kikosi cha Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa atamkosa kwa mara nyingine tena nyota wake Erling Haaland baada ya kuumia tena.
Guardiola amesema watamkosa Haaland hadi mwezi wa pili pindi majeraha yake yatakapokuwa yamepona.
“Haaland amekutana na changamoto kadhaa baada ya kutoka kwenye majeraha, na anaweza kurejea tena mwezi ujao”.
“Tunamhitaji arejee ili walau acheze miezi mitatu au minne ya mwisho bila kupata majeraha”.
“Nafikiri hadi mwishoni mwa msimu huu atakuwa tayari, ni mfupa, anahitaji muda, tumemkumbuka sana”.