Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane amelalamika swala la mechi za AFCON kuchezwa saa nane za mchana kutokana na hali ya joto kali inayoendelea kwasasa nchini Ivory Coast.
Mane ameweka wazi kuwa upangaji wa michezo katika muda huo ulikuwa unafanyika kipindi cha Karne za nyuma na sio kwenye karne hii na kusisitiza kuwa wanawanyima ladha ya mpira mashabiki zao kutokana na uchovu.
“CAF inabidi iachane na hizi ratiba za kupanga mida ya Michezo kama bado tupo Karne za nyuma, huko tushapita na maeneo mengi washaachana na swala la kupanga mechi kuchezwa Mchana wa Saa 8”.
“Wote tunaelewa hali ya hewa hapa Afrika, maeneo mengi ni Joto Kali, wachezaji tunachoka na wakati mwengine tunautumia muda mwingi kuwaza muda wa Mapumziko kuliko mbinu”.
“Tunawanyima ladha ya mpira mashabiki zetu kwasababu ya uchovu.. hata wanaotazama kwenye TV sidhani kama wanafurahia Mechi kuchezwa Saa 8 mchana”, Maneno ya mchezaji wa Timu ya Taifa la Senegal, Sadio Mane.
Michezo kadhaa ya AFCON msimu huu inachezwa saa nane mchena ambapo kwa Afrika Mashariki ni sawa na saa kumi na moja [17:00] Jioni.
Hivyo imekuwa ikiwaladhimu makocha kusimamisha mara kadhaa michezo na kuwapa nafasi ya kupooza miili wachezaji kwa maji kabla ya kuendelea tena.