AFCON

STARS HAITISHWI SANA NA MOROCCO KUELEKEA MECHI YA LEO.

Published on

Timu ya Taifa ya Tanzania leo inashuka Dimbani kuikabili timu ya Taifa ya Morocco majira ya saa mbili usiku katika mji wa San Pedro.

Uwanja utakaoikaribisha mechi hiyo ni Laurent Pokuo.

Morocco ni timu ya 13 kwa ubora Duniani huku Tanzania ikiwa nafasi ya 121 Duniani.

Adel Amrouche [Taifa Stars] na Walid Regragui [Morocco] wamekutana mara moja pekee na Walid ameshinda mchezo huo uliochezwa katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Timu hizi mbili kiujumla zimekutana mara tatu [3], Tanzania imeshinda mara moja [1] na Morocco imeshinda mara mbili [2].

Morocco imeifunga Tanzania magoli matano [5] katika michezo hiyo mitatu huku Tanzania ikiifunga Morocco magoli manne [4].

Hazijwahi kukutana kwenye mashindano haya makubwa ya fainali za mataifa ya Afrika, hii itakuwa ni mara ya kwanza kukutana.

Mchezaji wa kuchungwa zaidi kwenye mchezo wa leo kwa upande wa Morocco ni Hakim Ziyech na Youssef El-Neysri ambao wanaweza kubadili ubao wakati wowote.

Wachezaji wa kuchungwa zaidi upande wa Tanzania hii leo ni Mbwana Samatta na Simon Msuva ambao pia wana uwezo wa kufanya makubwa zaidi kwenye mchezo huu wakati wowote ule.

Tanzanina ina wastani wa umri wa wachezaji wa miaka 25.4 huku Morocco ikiwa na wastani wa umri wa 26.6, hivyo Tanzania ina vijana wengi zaidi ya Morocco.

Katika michezo mitano ilitopita Morocco imeshinda michezo minne [4] na kutoa sare mchezo mmoja [1] haijapoteza mchezo wowote, mara ya mwisho kupoteza ilikuwa dhidi ya Afrika Kusini [2-1], June 17, 2023.

Morocco katika michezo mitano iliyopita imefunga magoli kumi [10], imefungwa magoli mawili [2].

Tanzania kwenye michezo mitano iliyopita imeshinda michezo miwili [2], imepoteza michezo miwili [2] na kutoa sare mchezo mmoja [1].

Tanzania katika michezo mitano iliyopita imefunga magoli mawili [2] na imefungwa magoli manne [4].

Popular Posts

Exit mobile version