Nyota wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Zambia Clatous Chama amewashukuru mashabiki wa soka nchini Tanzania kwa nguvu wanayoendelea kumuonyesha.
Chama pia ameweka wazi kuwa kwenye mashindano haya wanaichukulia Zambia “Under dog” na ndio kitu ambacho wao wanataka ili wawaonyeshe kuwa wamejipanga kwaajili ya mashindano haya.
“Mimi binafsi nategemea mambo mengi kutoka AFCON, nashukuru Mungu nipo”.
” Sisi kama timu tunajua hatupo kwenye nafasi nzuri kwasababu wanatuchukulia kama “Underdog”, na hicho ndio tunataka”.
“Timu yetu nzima tunataka kuwa timu ya ushindi, timu ambayo itashindana na timu ambazo zinatarajiwa kufanya vizuri”.
“Na sisi tunaombea tuweze kutwaa ubingwa”.
“Mashabiki wa Tanzania nawashukuru sana kwasababu wananiunga mkono sana, na kunipa upendo mkubwa sana, naomba tu watuombee kama timu na mimi kama mchezaji niifurahie hii michuano”.
Amezungumza Clatous Chota Chama, nyota wa Zambia na klabu ya Simba ya Tanzania.
Zambia itakuwa na kibarua hii leo majira ya saa tano usiku kuikabili timu ya Taifa ya Congo DR kwenye mchezo wa kundi F.