Mchezo mwingine wa usiku sana majira ya saa tano [23:00] usiku utazikutanisha timu ambazo zimewashangaza watangazaji wengi na wapenzi wa soka kwa kupata matokeo ambayo hawakutegemea hadi zilipofika hatua hii.
Hizi ni takwimu za timu hizi kuelekea mchezo huu wa leo kati ya Afrika Kusini dhidi ya Cape Verde hii leo.
•Cape Verde na Afrika Kusini zinakutana kwa mara ya pili kwenye fainali za mataifa ya Afrika, mara ya kwanza walitoka sare ya 0-0 kwenye hatua ya makundi mwaka 2013, Afrika Kusini walikuwa waandaaji wa michuano hiyo.
- Afrika Kusini Wamefika hatua ya robo fainali mara tatu katika mara nne walizoshiriki mashindano haya, wanasaka nafasi ya kufuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 walipopoteza dhidi ya Nigeria.
- Cape Verde wameshinda michezo mitatu [3] kwenye AFCON 2023, wamefunga magoli nane [8].
- Cape Verde wanatafuta nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza katika mara mbili walizofuzu hatua ya robo fainali, mara ya kwanza tangu walipochapwa 2-0 dhidi ya Ghana 2013.
- Afrika Kusini imeondoka na hati safi [Clean Sheet] tatu kwenye michuano hii kwa mara ya kwanza tangu February 1998, Bafana Bafana hawajawahi kuacha kifunga kwenye mechi nne za AFCON mfululizo.
- Afrika Kusini wamefanya mabadiliko mawili kwenye kikosi chao cha kwanza kwenye AFCON 2023, wapinzani wao Cape Verde wamefanya mabadiliko 14 ni Guinea pekee iliyofanya mabadiliko mengi kwenye kikosi chao [17].
- Cape Verde inawastani mkubwa wa umri miak 29 na siku 64 kwenye michuano hii ya AFCON 2023, magoli matano [5] kati ya nane [8] yamefungwa na wachezaji wenye umri wa kuanzia miaka 30, timu ya mwisho kufunga magoli mengi kutoka kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30+ ilikuwa ni Misri mwaka 1998 wakifunga magoli saba [7].
- Themba Zwane amehusika kwenye magoli matatu [3] kati ya sita [6], ya Afrika Kusini msimu huu [Amefunga Magoli mawili na kutoa pasi moja], atakuwa mchezaji wa kwanza kuhusika kwenye magoli mengi tangu afanye hivyo Shaun Bartlett mwaka 2000 [5].
- Ryan Mendes amehusika kwenye magoli mengi [4], Pasi mbili [2] za mwisho na Magoli mawili [2], kuliko mchezaji yoyote wa Cape Verde kwenye michuano ya AFCON.