Makala Nyingine

UWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.

Published on

Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe la Dunia la mwaka 2026 ambalo litaandaliwa na nchi tatu kwa pamoja za Amerika Kaskazini.

Shamrashamra na mchezo wa ufunguzi wa fainali za kombea Dunia mwaka 2026 zitafanyika nchini Mexico, June 11, 2026.

Sherehe hizo kubwa za soka Duniani zitafanyika katika uwanja wa Estadio Azteca uliopoa Jijini Mexico na mchezo wa kwanza utaishuhudia timu ya Taifa ya Mexico ikishuka Dimbani.

Ikumbukwe fainali hizo zinatarajiwa kufanyika nchi tatu, Canada, Mexico na Marekani. Wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu uwanja huo kutumika kwaajili ya ufunguzi.

” Pele alibeba kombe la Dunia 1970 na Maradona 1986 kwenye uwanja huu huu, sasa ni zamu ya Cristiano Ronaldo 2026, ngoja niendelee kuota”. Alisema shabiki wa kwanza.

“Huu ndio uwanja wenye historia kubwa na mpira wa miguu”, Shabiki wa pili alizungumza.

“Ilitakiwa mchezo wa ufunguzi upigwa Canada kwani hawajawahi kuwa wenyeji wa michuano hii, FIFA imetusikitisha”, alizungumza shabiki wa tatu.

“Twendeni, mimi sitokei Mexico lakini kinaenda kuwa kipindi bora sana”, alisema shabiki wa nne.

“Ilitakiwa iwe fainali”, alimaliza shabiki wa tano kuzungumza.

Uwanja huu wa ufunguzi una historia kubwa na kombe la Dunia kwani mwaka 1970 mchezaji bora wa Dunia kipindi hicho alibeba kombe hilo akiwa na timu yake ya Taifa ya Brazil.

Mwaka 1986 mchezaji bora mwingine Duniani Diego Maradona akatwaa ubingwa wa kombe la Dunia katika uwanja huo huo akiwa na timu ya Taifa ya Argentina.

Wadau wanaamini huenda fainali hizi zikampa nafuu nyota wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, yakajirudia yale ya zamani kuwa wachezaji wote bora wawili wa Dunia kwa kipindi husika wanatwaa kombe la Dunia.

Mchezo wa fainali utapigwa nchini Marekani July 19, 2026 katika uwanja wa Newyork New Jersey uliopo Jijini New York.

Mchezo wa ufunguzi nchini Marekani utapigwa June 12, 2026 kwenye uwanja wa Los Angeles huku tarehe hiyo hiyo Canada pia itakuwa dimbani kwenye uwanja wa Toronto.

Popular Posts

Exit mobile version