AFCON

HUGO: ILI USHINDE AFCON USICHEZE VIZURI.

Published on

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Afrika Kusini Hugo Broos ameweka wazi kuwa ili uweze kushinda michezo ya Afcon haupaswi kucheza vizuri.

“Mechi dhidi ya Cape Verde tulishinda lakini hatukucheza vizuri, dhidi ya Nigeria tumecheza vizuri na wao hawakuwa vizuri lakini hatujashinda na wao wameshinda, huo ndio Mpira”.

“Nawapongeza wachezaji wangu wamejituma na sasa tunahamashia nguvu kwenye Michezo ya kutafuta kufuzu Kombe la Dunia.”

Maneno ya Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Afrika Kusini, Hugo Broos baada ya Mchezo wa jana dhidi ya Nigeria.

Afrika Kusini ilitolewa na timu ya Taifa ya Nigeria kwa changamoto ya mikwaju ya Penalty baada ya sare ya kufungana goli 1-1 kwa dakika zote 120.

Popular Posts

Exit mobile version