AFCON

FAINALI, IVORY COAST vs NIGERIA.

Published on

Ivory Coast watakuwa na lengo la kukamilisha hadithi yao ya Kombe la Mataifa ya Afrika hapo baadae watakapocheza na Nigeria katika fainali itakayopigwa katika Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Ebimpe, Abidjan.

Wakati Ivory Coast (Tembo wa Afrika) watakuwa wakilenga kutwaa taji la tatu la michuano ya Afcon, Nigeria (Super Eagles) watakuwa wakiwinda taji lao la nne la Afcon.

Wenyeji walinusurika kuondolewa mapema kabisa lakini wakapita katika hatua ya mtoano kwa mgongo wa (best looser) na kuendelea kuwaondoa mabingwa watetezi Senegal, Mali na DR Congo kuelekea katika mchezo wa fainali.

Washindi wa 2013 waliifunga Cameroon katika hatua ya 16 bora, kabla ya kuwashinda Angola na Afrika Kusini na leo wanatarajia kucheza mchezo wa fainali na wenyeji Ivory Coast.

Unatarajiwa kuwa mchuano mkali na mashabiki wanauhakika wa kupata burudani safi.

Dauda Sports imekuandalia mambo yote hapa ili kukuwezesha kukupa taswira kuelekea katika mchezo huu wa fainali.

TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA.

Terem Moffi na Kelechi Iheanacho walipata nafasi ya kuonesha thamani yao katika michuano hii ya Afcon.

Moffi alipewa jukumu muhimu baada ya kutolewa nje kwa Grant Kekana katika nusu fainali dhidi ya Afrika Kusini huku Kelechi Iheanacho akifunga mkwaju wa penati katika mchezo huo.

Bright Osayi-Samuel anatarajiwa kuanza katika nafasi ya beki wa kulia mbele ya Zaidu Sanusi.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST.

Nwabali, Ajayi, Troost-Ekong, Bassey, Osayi-Samuel, Onyeka, Iwobi, Aina, Simon, Lookman, Osimhen.

TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST.

Beki wa kulia wa Nottingham Forest Serge Aurier anaweza kupangwa kwenye kikosi cha kwanza baada ya kukosa nusu fainali DR Congo kutokana na kadi tatu za njano alizozipata kwenye michezo ya awali.

Oumar Diakite pia amerejea kutoka kusimamishwa huku Sebastien Haller ambaye yuko fiti tena anatarajiwa kuongoza idara ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Mshambulizi mwenye uzoefu Max Gradel ana uwezekano mkubwa wa kuanza mbele ya Nicolas Pepe.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA.

Fofana, Aurier, Boly, Ndicka, Konan, Kessie, Seri, Fofana, Pepe, Haller, Adingra

TAKWIMU ZA TIMU HIZI MARA YA MWISHO KUKUTANA.

Ivory Coast ndiyo timu iliyohamasishwa zaidi mara baada ya kuanza vibaya kwa mashindano, hawana cha kupoteza. Waliifunga Mali 1-0 katika nusu fainali na kusonga mbele.

Nigeria iko chini ya shinikizo la kuirudisha heshima ya Taifa lao mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11, walipata ushindi wa 4-2 kwa mikwaju ya penati ili na kuiondoa Afrika Kusini katika mashindano baada ya sare ya 1-1 baada ya kanuni ya muda wa ziada.

Hii ni mara ya tano kwa mataifa haya mawili kukutana katika Afcon tangu 2006. Kila timu ikishinda mara mara mbili, hakuna sare, huku leo ikitazamiwa kuamua ni nani kati ya haya mataifa mataifa mawili atakuwa mbabe dhidi ya mwenzake.

Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana ni katika michuano hii ya Afcon inayoendelea ambapo Nigeria (Super Eagles) walishinda kwa bao la pekee lililofungwa na William Troost-Ekong.

Popular Posts

Exit mobile version