Nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Uholanzi Quincy Promes amehukumiwa kwenda jela kwa miezi sita kwa kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine kilo 1350.
Promes alitakiwa kwenda jela miaka tisa lakini akapunguziwa zaidi na kuhitajika kutumikia miaka sita pekee na mahakama ya nchini Uholanzi lakini nyota huyo hakuwepo siku ya hukumu.
Nyota huyo kwasasa anaitumikia klabu ya Spartak ya Urusi, nyota huyo bado anaendelea kudai kuwa hakufanya kosa hilo, kwasasa anajiandaa kukata rufaa juu ya hukumu hiyo, tukio hilo linadaiwa kufanyika January 2020 alipokuwa akiitumikia Ajax ya Uholanzi.
Urusi huwa haijishughulishi na chohote kuhusiana na raia wa Uholanzi, hii inamaanisha kuwa Promes anaweza kuendelea na kazi yake ya kuitumikia Spartak kama atakataa kurudi nyumbani Uholanzi.
Hii sio mara ya kwanza kwa winga huyo kukutwa na hatia ambapo awali alihukumiwa miezi 18 jela baada ya kumdharirisha binamu yake kwenye sherehe mwaka mmoja uliopita.
Spartak itashuka dimbani wiki ijayo siku ya Jumatano dhidi ya Kairat, tunasubiri kuona kama Promes atahusika na mchezo huo.