Mfungaji bora wa michuano ya AFCON 2023 Emilio Nsue [34] amesimamishwa kuitumikia timu ya Taifa ya Equatorial Guinea baada ya kuonyesha utovu mkubwa wa nidhamu mara baada ya timu yao kuondolewa mashindanoni.
Nyota mwingine pia wa timu hiyo Salvador, 28, nae pia amesimamishwa kuitumikia timu hiyo ya taifa ya Equatorial Guinea baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu wakati wakiwa nchini Ivory Coast.
Salvador alikutwa na hatia na askari nchini Ivory Coast kwenye mji wa Abidjan kitu ambacho shirikisho limesema ni kuliaibisha Taifa na timu yao.
Nyota hao wawili hawatahusika kwenye timu hiyo hadi pale uchunguzi utakapokamilika ndipo watarejeshwa tena kwenye kikosi hicho, hata hivyo utovu huo wa nidhamu haujawekwa wazi.
Nsue alimaliza kinara wa upachikaji magoli kwenye fainali za mataifa ya Afrika baada ya kufunga goli tano [5] kwenye michezo minne [4] ambayo timu yake ilicheza.
Nsue alifunga magoli matatu [Hattrick] kwenye mchezo dhidi ya Guinea Bissau na kufunga magoli mawili [2] zaidi kwenye mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Bingwa wa michuno hiyo timu ya Taifa ya Ivory Coast.
Equatorial Guinea iliondolewa hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON 2023 baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Guinea.