Top Story

ASITISHIWA MKATABA KISA KUJISAJILI MTANDAO WA MAHUSIANO.

Published on

Klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki imevunja mkataba na kiungo wake mshambuliaji Emirhan Delibas (21) baada ya wasifu wake kuonekana kwenye mtandao wa ngono kabla ya kuenea kwenye mitandao ya kijamii.

Emirhan ameachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya nyota huyo kukataa kuwa akaunti haikuwa yake licha ya kuwa picha ilikuwa yake na kuiita kuwa ni “Fake Account”.

Klabu imeandika kuwa “Tumeachana na mchezaji wetu Emirhan Delibas kwa makubaliano ya pande zote mbili, tuna mtakia kila lakheri kwenye maisha yake ya soka”.

Kwenye wasifu wa ukurasa huo wa ngono kuna picha ya Delibas akiwa amevaa jezi ya mazoezi ya Besiktas huku ameshikilia kinywaji, jina lake na umri wake wa uongo unaosoma miaka 24.

Nyota huyo ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram “Nina pingana na huo upuuzi uliofanywa na akaunti fake, upendo wangu kwenye timu hii sio wa kuuliza”.

“Besiktas ni majukumu yangu, upendo wenu umekuwa ukinipa nguvu ya kupambana sana”.

Delibas amecheza michezo miwili pekee kwenye timu ya wakubwa hadi mkataba wake unasitishwa, alicheza dhidi ya Kasimpas kwenye mchezo wa Ligi ambao timu hiyo ilipoteza akicheza dakika tisa na mchezo wa Europa Conference League dhidi ya Cameo.

Ameaza kutumika kwenye timu za vijana tangu mwaka 2010 akiwa na miaka saba kabla ya kuanza kucheza timu ya wakubwa mwaka 2020.

Delibas amecheza timu za vijana za timu ya Taifa ya Uturuki kwa umri U-17, U-18, na U-19.

Popular Posts

Exit mobile version