Shirikisho la soka nchini (TFF) limetuma barua CAF ya kieleza kuwa mechi ya Yanga dhidi Mamelodi Sundowns itachezwa kwa kanuni na taratibu za soka zilizowekwa na namna ya kuingia uwanjani, kigezo sio passport.
“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linalihakikishia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa mechi husika itachezwa kwa kanuni na taratibu zilizowekwa za soka na namna ya utaratibu wa kuingia uwanjani.”- Taarifa ya barua ya TFF.
“Kwa hivyo, sio kwamba pasipoti (pasi za kusafiria) zitatumika kama kigezo cha kuingia uwanjani kwa mashabiki wa Mamelodi Sundowns na mtu yeyote kwa sababu mechi ipo kikanuni na taratibu za mpira wa miguu bali sio kwa Idara ya Uhamiaji.”- Taarifa ya barua ya TFF.
“Timu ya Mamelodi Sundowns imehakikishiwa usalama wao kutoka kwa vyombo husika wakati wote ambao watakuwa nchini na kuheshimu taratibu za mechi yao dhidi ya Young Africans SC, na Dhamana hii pia inawahusu maafisa wa mechi, mashabiki wa Sundowns wanaosafiri pamoja na mashabiki wanaoishi Tanzania na anaetaka kuhudhuria mechi hiyo.” – Taarifa ya barua ya TFF.
Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani afrika dhidi ya Mamelodi sundowns utakaopigwa Jumamosi, March 30 katika dimba la Benjamini mkapa saa tatu [21:00] usiku.