Mshambuliaji wa klabu ya Al Ahly Mahmoud Sulaiman Kahraba ameweka wazi kuwa ndoto yake ilikuwa kuichezea Al Ahly tangu akiwa Zamalek.
Pengine hii ni miongoni mwa kauli ambazo mashabiki wa klabu ya Zamalek hawapendi kabisa kuisikia na hawakutaka kuisikia kutoka kwa nyota ambaye wao walimlea.
“Kusajiliwa Al Ahly ni moja ya jambo zuri zaidi ambalo limewahi kutokea kwenye maisha yangu, mimi ni Al Ahly hata wakati nikiwa Zamalek.” – Kahraba.
Zamalek na Al Ahly ni wapinzani wa kutupwa nchini Misri, na haiwezi kutokea hata siku moja shabiki wa Al Ahly akaenda kumuunga mkono Zamalek na upande hivyo hivyo.