Fenerbahce

FRNERBAHCE KUPIGA KURA YA KUISUSIA LIGI KUU LEO.

Published on

Klabu ya Fenerbahce ina mpango wa kupiga kura leo Jumanne kama waendelee na msimamo wao wa kutoshiriki Ligi kuu nchini Uturuki ama laah.

Uamzi huo unakuja baada ya wachezaji wao kuvamiwa na mashabiki uwanjani kwenye mchezo wao dhidi ya Trabzonapor uliomalizika kwa ushindi wa goli 3-2.

Kitendo cha kuingia uwanjani mashabiki na kufanya fujo kilimuibua pia Rais wa shirikisho la soka Duniani Giann Infatino ambaye aliagiza hatua kali zichukuliwe kwa wote waliohusika.

Hata hivyo hadi hivi sasa shirikisho la soka nchini Uturuki bado halijatoa tamko lolote kitendo ambacho kinawafanya Fenerbahce wafanye maamuzi hayo magumu.

Popular Posts

Exit mobile version