Al-Nassr

RONALDO KUANDIKA REKODI MPYA MWISHO WA MSIMU HUU.

Published on

Nyota wa klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo anaweza kuandika historia ya kuwa nyota aliyebeba kiatu cha ufungaji bora kwenye Ligi kubwa nne Duniani, rekodi ambayo haijawahi kuandikwa na mchezaji yoyote Duniani.

Ronaldo kwasasa anaongoza kwa upachikaji wa magoli kwenye Ligi ya Saudi Arabia akiwa na magoli 26 huku akifuatiwa na Aleksandar Mitrovic wa Al Hilal mwenye magoli 22 ambaye hata hivyo amemaliza msimu wake baada ya kuumia.

Ronaldo alibeba kiatu cha ufungaji bora England [EPL] akiwa na Manchester United, Hispania [Laliga] akiwa na Real Madrid, Italia [Serie A] akiwa na Juventus na inawezekana tena sasa Saudi Arabia akiwa na Al Nassr.

Mwaka 2016 gazeti la The Guardian lilichapisha kuwa nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil Romario alibeba kiatu cha ufungaji bora Hispanoa, Uholanzi na Brazil na aliwahi kufanya hivyo pia kwenye Ligi daraja la kwanza Brazil.

Nyota wengine waliowahi kutwaa kiatu cha ufungaji bora kwenye nchi tatu tofauti ni Alfredo De Stefano, Ruud Van Nistelrooy, na Robert Lewandowski.

Nyota mwingine ni Luis Suarez, alitwaa Uholanzi [Eredivisie] akiwa na Ajax, Laliga akiwa na Barcelona na EPL akiwa na Liverpool, Suarez kwasasa ana magoli matano kwenye michezo saba ya klabu ya Inter Miami inayoshiriki MLS nchini Marekani.

Ronaldo anaweza kuwahi kuvunja rekodi hiyo mbele ya Suarez kutokana na msimu wa Saudi Arabia kuwahi kumalizika mapema huku Msimu wa Marekani utafika tamati mwezi October.

Popular Posts

Exit mobile version