CAF Champions League

“AL AHLY IMECHOKA” – NYOTA PYRAMIDS AWATONYA SIMBA.

Published on

Klabu ya Simba leo itatupa karata yake ya mwisho ya kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika nchini Misri dhidi ya Al Ahly.

Simba inahitaji kupata walau goli moja ili ifufue matumaini ya kusonga mbele baada ya mchezo awali uliopigwa Dar Es Salaam kupokea kichapo cha goli 1-0.

Simba iliyo chini ya kocha aliyebeba ubingwa wa kombe la shirikisho msimu uliopita mbele ya Yanga Abdelhakh Benchikha ina kibarua kizito leo majira ya saa tano [23:00] usiku.

Licha ya kuwa Simba imepoteza mchezo wake wa awali lakini mashabiki wake wana matumaini ya kufanya vyema kwenye ardhi ya ugenini kutokana na morali ya wachezaji waliyonayo.

Nyota wa zamani wa klabu ya Yanga ambaye kwasasa anaitumikia klabu ya Pyramids ya nchini Misri, Fiston Mayele alipata nafasi ya kuitembelea klabu ya Simba mara baada ya kutua nchini Misri.

Mayele katika mahojiano na Simba TV akaeleza kuwa kwasasa Al Ahly haitishi kama zamani na haina ubora ule wa zamani kutokana na wachezaji wake wengi kuwa wamechoka.

“Al Ahly ya zamani sio kama ya sasa, unajua hawajabadilisha sana wachezaji na wachezaji nao ni binadamu hivyo wanachoka”.

  • Fiston Mayele – Nyota wa Pyramids

Simba hii ni mara ya kwanza inakutana na Al Ahly kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Popular Posts

Exit mobile version