Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameonyesha wazi furaha yake juu ya kuondolewa klabu ya Yanga kwenye hatua ya Robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika.
Ahmed ameeleza kuwa Mamelodi Sundowns wamekuwa na kawaida ya kuishia robo fainali mara zote kama ilivyo kwa Simba lakini kwakuwa walijipatia kibonde wake wakajichapia.
“Nimefurahi kwasababu nilitaka waone ni ngumu kiasi gani kufuzu kutoka hatua ya robo fainali kwenda hatua ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.”
“Tena wao washukuru wamecheza na timu ambayo haina uzoefu wa kufuzu kutoka robo fainali kwenda nusu fainali, Mamelodi wanaishiaga robo fainali kama sisi tu.”
- Ahmed Ally, Afisa Habari Simba
Simba na Yanga zote ziliondolewa kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika msimu wa 2023/24.
Simba ndio timu pekee kwenye hatua ya robo fainali iliyotolewa kwa kufungwa kwenye michezo yote miwili, wakifungwa 1-0 Dar Es Salaam na wakafungwa 2-0 Cairo dhidi ya Al Ahly.
Yanga iliondoshwa kwa changamoto ya mikwaju ya Penalty na Mamelodi Sundowns baada ya michezo yote miwili kumalizika kwa suluhu Dar Es Salaam na Pritoria, Afrika Kusini.