Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania kwa Walemavu, Tanzania Amputee Football National team maarufu kama Tembo Warriors wapo tayari kwa ajili ya mashindano ya AAFCON(AFRICAN AMPUTEE FOOTBALL CUP OF NATIONS) yanayotarajiwa kutimua vumbi kuanzia Tarehe 19-28 Aprili 2024.
Tanzania imepangwa Kundi D ikiwa sambamba na Angola, Sierra Leone na Rwanda na wanatarajia kucheza mechi ya Kwanza Tarehe 20 Aprili dhidi ya Rwanda.
AAFCON ndiyo itakayotoa tiketi kwa timu zitakazoenda kushiriki Kombe la Dunia, WAFF 2026 huku ikiwa ndio mara ya kwanza mashindano haya kufanyika barani Afrika.
Itakumbukwa kulitokea taarifa ya kuhairishwa mashindano haya mpaka mwezi Mei 2024 kutokana na sababu za kiusajili zikitajwa haswa lakini mpaka sasa bado ratiba inasema mashindano haya yatatimua vumbi kama yalivyopangwa.