Ligi ya Taifa ya mchezo wa mpira wa kikapu(NBL-National Basketball League) msimu huu wa 2023 inatarajiwa kuingia kwenye mzunguko wa 3 leo ukishuhudia michezo kadhaa ikipigwa kwenye viwanja mbalimbali jijini Dodoma.
Katika mchezo wa jana wa mwisho wa mzunguko wa pili, uliishuhudia timu ya Dar City Basketball ambao ndio mabingwa wa mkoa wa Dar es Salaam wakiichapa Kisasa Heroes ya Dodoma kwa vikapu 49-43 kwenye mchezo uliotawaliwa na tambo nyingi sana nje na ndani ya uwanja.