Anakosekana Yao Attohoula hivyo Dickson Job atacheza upande wa kulia kama ilivyo kwa Lomalisa upande wa kushoto wa ulinzi. Ibrahim Bacca anarejea kikosini kucheza sambamba na Nahodha, Bakari Mwamnyeto.
Maxi Nzengeli , Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki kwa pamoja utatu huu utakuwa na jukumu la kummlisha Kijana Clement Mzize akicheza kama Mshambuliaji pekee. Huku Mudathir Yahya na Khalid Aucho wakifanya kazi chafu ya kiungo wa Ulinzi.
Feisal Salum amekuwa kwenye moyo wa haya yote mara nyingi akicheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho, Prince Dube. Safu ya Kiungo cha ushambuliaji itakamilishwa na Abdul Sopu na Djibril Sylla. Sospeter Bajana na Akaminko wanatarajiwa kuwepo kwenye Mhimili kuwapa ulinzi safu yao ya Ulinzi, ikiwa na Lusajo Mwaikenda, Cheikh Sidibe, Malickou Ndoye na Nahodha Daniel Amoah kumlinda Idrissu.