Stephen Curry usiku wa kuamkia leo, ameweka rekodi nyingine kwa kufikisha michezo 250 akifunga alama 3(3 Points shot) mfululizo kwenye ushindi mgumu wa 102-101 dhidi ya Sacramento Kings.
Curry ameendelea alipoishia msimu uliopita kwa kuiongoza timu yake kupata ushindi huo wa 4 msimu huu akifunga alama 21 kwenye dakika 32 alizocheza.
Kwingineko huko Los Angeles, LeBron James aliendelea kuiongoza timu yake ya LA Lakers kuwafunga watani na majirani wao LA Clippers vikapu 130-125 kwenye Muda wa ziada(Over Time).
James alifunga vikapu 35, Akirejesha mipira(Rebounds) mara 12 na kutoa pasi za usaidizi(Assists) 7 kwenye dakika 42 alizocheza. James akicheza na vijana wengi kama Austin Reeves na Christian Wood iliwalazimu kushinda kwenye OT baada ya kwenda sare kwenye muda wa kawaida.