NBA wanaenda kuzindua msimu wa kwanza wa PLAY- IN TOURNAMENT, ikishirikisha timu zote 30 zinazocheza msimu wa kawaida wa NBA 2023/24 yanayotarajiwa kuanza leo Nov 3-Disemba 7.
PLAY-IN TOURNAMENT itahusisha makundi 6 yaliyogawanya makundi matatu kwenye kanda zote mbili, Mashariki na Magharibi.
NBA walisema kuwa wanatamani kutafuta mashindano ambayo yatakuwa na ushindani zaidi mapema kabisa na sio mpaka mashabiki wasubiri hadi karibia na Krisimasi kutazama PLAY- OFFS. Hata hivyo ukiacha matokeo ya Fainali, matokeo mengine yote ya michezo itaathiri pia misimamo ya ligi ya misimu ya kawaida.
Washindi wa makundi yote 6, wataunganishwa na timu 2 zilizofanya vizuri zaidi baada ya washindi kupatikana na kupata timu 8 zitakazocheza Robo Fainali kati ya tarehe 4-5 Disemba, kisha kufuatiwa na Nusu Fainali na Fainali tarehe 7 Disemba.
Mechi za awali kila Timu itakutana na wapinzani wake wanne kwenye kundi 1 la timu 5. Mechi za mtoano kutakuwa na mechi mbili za nyumbani na Ugenini.
Zawadi zitatolewa kama kawaida kwa washindi wa jumla hadi washindi binafsi ikiwemo MVP.
Makundi ya NBA PLAY- IN TOURNAMENT 2023 ni kama ifuatavyo
MAGHARIBI
Kundi A: Memphis Grizzlies, Phoenix Suns, LA Lakers, Utah Jazz, Portland Trail Blazers
Kundi B: Denver Nuggets, LA Clippers, New Orleans Pelicans, Dallas Mavericks, Houston Rockets
Kundi C: Sacramento Kings, Golden State Warriors, Minnesota Timberwolves, Oklahoma City Thunder, San Antonio Spurs
MASHARIKI
Kundi A: Philadelphia 76ers, Cleveland Cavaliers, Atlanta Hawks, Indiana Pacers, Detroit Pistons
Kundi B: Milwaukee Bucks, New York Knicks, Miami Heat, Washington Wizards, Charlotte Hornets
Kundi C: Boston Celtics, Brooklyn Nets, Toronto Raptors, Chicago Bulls, Orlando Magic
Ratiba ya michezo ya leo tumekuwekea hapo juu. Muda wote ni Jumlisha Masaa 7.