NBA

BILA LEBRON JAMES, LAKERS WATAKATA NBA

Published on

Los Angeles Lakers walipata ushindi wa 116-110 dhidi ya Portland Trail Blazers kwenye mchezo wa ligi ya kikapu nchini marekani, NBA,  licha ya kummkosa nyota wao LeBron James, kwenye mchezo ambao watu wengi waliibeza Lakers kwa kubebwa na waamuzi.

Alikuwa ni  Antony Davis na Austin Reaves ndio waliiteka shoo ya Lakers, akifunga vikapu 30, pasi za usaidizi 6 na kurejesha mipira mara 13 kwenye dakika 41 alizocheza.

Lakers wanapata ushindi wa pili mfululizo wiki hii baada ya kupata ushindi wa 122-119 kwenye NBA In-Season Tournament dhidi ya Phoenix Suns, jumamosi. Ushindi huu unafikisha 5-5, yani Ushindi wa 5 msimu huu na kupoteza  5 kwa Lakers ambayo bado inaonekana kujitafuta.

Matokeo mengine ya NBA Regular Season Jana ni kama ifuatavyo

Warriors walifungwa 110-116 na Minnesota Timberwolves, Phoenix Suns wakiwa nyumbani nao walibugizwa vikapu 111-99 na Oklahoma City Thunder, Chicago Bulls walishinda 119-108 Detroit Pistons huku New Orleans pelicans waliruhusu kipigo cha 124-136 nyumbani kutoka kwa Dallas Mavericks.

Kwingineko Victor Wembanyama na San Antonio Spurs yake walifungwa vikapu vya 118-113 na Miami Heat, Bam Adebayo akiiba shoo. Philadelphia 76ers walishinda kwa vikapu 137-126 dhidi ya Indiana Pacers, huku Houston Rockets wakiwafunga Dever Nuggets kwa vikapu 107-104.

Michezo mingine kuendelea Usiku wa kuamkia kesho itawakutanisha, Toronto Raptors v Washington Wizards, Boston Celtics v New York Knicks, Milwaukee Bucks v Chicago Bulls na Sacramento Kings v Cleveland Cavaliers.

Popular Posts

Exit mobile version