Giannis Antentokoumpo usiku wa kuamkia leo, aliifungia timu yake ya Milwaukee Bucks vikapu 35 na kuisaidia timu yake kupata ushindi wake wa 7 msimu huu wa NBA.
Giannis alipata Double-Double akirejesha pia mipira 11 huku akitoa pasi za usaidizi 2 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa sana ambapo timu yake ilishinda kwa jumla ya vikapu 118-109 dhidi ya Chicago Bulls. Alama zingine zikichangiwa na Khris Middleton(13) na Damian Lillard(12).
Matokeo mengine ni pamoja na :
Sacramento Kings kuwafunga Cleveland Cavaliers 132-120. Pascal Siakam alifunga vikapu 39, kurejesha mipira mara 11 na pasi za usaidizi 7 kuisaidia timu yake ya Toronto Raptors kuwanyuka Washington Wizards, 111-107. Boston Celtics walipata ushindi wa 114-98 dhidi ya New York Knicks. Jason Tatum(35 vikapu) na Jrue Holiday(14 Vikapu) wakipeleka furaha kwa Celtics