Mapinduzi Cup

TIMU 12 KUSHIRIKI MAPINDUZI CUP 2024.

Published on

Michuano ya mapinduzi cup inatarajiwa kuanza kutimua vumbi December 28 mwaka huu ikihusisha timu 12 kutoka mataifa matano ya Afrika mshariki.

Timu nne [4] kutoka mataifa manne zimethibitisha ushiriki wake ikiwemo URA kutoka Uganda, Bandari kutoka Kenya, Vital’O kutoka Burundi, na APR kutoka Rwanda.

Timu nne kutoka visiwani Zanzibar ambazo ni KVZ, Mlandege, Chipukizi na Jamhuri, hizi zitaiwakilisha Ligi kuu visiwani Zamzibar kwenye michuano hii mikubwa ya kuadhimisha miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kutoka Ligi kuu kandanda Tanzania Bara itawakilishwa na vinara wa Ligi hiyo Young Africans, Simba, Azam FC pamoja na Singida Fountain Gate.

Sababu kubwa ya michuano hii kuchezwa mwezi December tofauti na vile ilivyokuwa imezoeleka huwa inachezwa mwezi January ni kupisha fainali za mataifa ya Afrika ambazo zitafanyika mwezi January nchini Ivory Coast huku Tanzania ikiwa miongoni mwa timu zitakazoshiriki fainali hizo.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni klabu ya Mlandege kutoka Visiwani Zanzibar iliyobeba ubingwa huo baada ya kuinyuka klabu ya Singida Fountain Gate 2-1 katika mchezo wa fainali msimu uliopita uliochezwa January 13 mwaka huu.

Popular Posts

Exit mobile version