Mapinduzi Cup

UWANJA WA AMAAN KUBADILISHWA JINA.

Published on

Waziri wa habari vijana utamaduni na Michezo wa Visiwani Zanzibar Mheshimiwa Tabja Maulid Mwita amemuomba Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuubadili jina uwanja wa Amaan kutoka kuitwa Amaan na kuwa Amaan Sports Complex.

Hii imekuja baada ya maboresho yaliyofanywa kwenye uwanja huo ambao mara nyingi umekuwa ukitumika kwenye mashindano ya mapinduzi.

“Niseme tu kwa niaba ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo tunachukua nafasi hii kukushukuru sana Mhe Rais kwa jitihada zako kubwa za kuhakikisha unaisimamia nchi yetu lakini kuhakikisha unaendeleza maeneo yote yanayohusu Habari, Vijana Utamaduni na Michezo”

“Tunaombi, wakati uliopita uwanja huu wa Amaan tukiwa na matukio tunasema tukutane Amaan Stadium, Mhe Rais tunaomba tubadilishe jina tuseme Amaan Sports Complex, eneo hili la Amaan lina kila sifa, lina kila sababu na lina kila vigezo kuitwa Amaan Sports Complex”

  • Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe Tabia Maulid Mwita

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanya jitihada kubwa sana za kuhakikisha miundombinu ya michezo inaboreshwa ili kuwapa nafasi vijana kuonyesha vipaji vyao.

Kwa kipindi kirefu sasa Zanzibar imekuwa ikizalisha wanamichezo bora ambao wamekuwa wakifanya vyema kwenye Ligi ya Zanzibar pamoja na Tanzania Bara.

Siku chache zilizopita kupitia uwekezaji kwenye michezo unaofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 15 ilitwaa ubingwa wa CECAFA michuano iliyofanyika nchini Uganda.

Popular Posts

Exit mobile version