Mapinduzi Cup

KOCHA APR ALIA NA MECHI NYINGI SIKU CHACHE.

Published on

Kuelekea mchezo wa robo fainali ya pili kati ya klabu ya Yanga na APR ya michuano ya kombe la mapinduzi hapo kesho kocha wa APR ameeleza namna ambavyo kikosi chake kinajiandaa.

Kocha mkuu wa kikosi cha APR ya Rwanda Thierry Froger ameweka wazi kuwa Yanga ni timu kubwa hivyo maandalizi yake yanapaswa kuwa ya tofauti kidogo.

“Maandalizi yataanza leo jioni, najua Yanga ni timu kubwa nchini Tanzania na ni miongoni mwa timu ambazo zinatazamiwa kunyakua ubingwa wa mapinduzi”.

“Nitajaribu kuongeza wachezaji wengine ambao hawakuonekana kwenye michezo iliyopita ili nguvu ziongezeke kwenye kikosi changu”.

“Kuna faida nyingi sana za kucheza mashindano haya, hasa hasa unapokutana na timu kubwa kutoka Tanzania, inasaidia kuboresha kwenye benchi letu la ufundi na kuboresha kiwango cha timu”.

“Mechi tatu ndani ya siku sita hata FIFA hairuhusiwi lakini tunaomba Mungu tusipate majeruhi, ni ngumu sana kwa wachezaji wake kucheza mechi nyingi kwa wiki moja”.

APR itashuka dimbani kesho saa 2:15 usiku kuikabili klabu ya Yanga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi inayoendelea huko visiwani Zanzibar.

Popular Posts

Exit mobile version