Tanzania imepanda nafasi mbili juu kwenye viwango vya shirikisho la soka Duniani FIFA kwa mwezi wa pili [February] zilizotolewa hii leo.
Tanzania kabla ya kupanda ilikuwa nafasi ya 121 ikiwa na alama 1155.19 na sasa imepanda hadi nafasi ya 119 ikifikisha alana 1160.98.
Tanzania imeongeza alama 5.79 kutokana na kiwango walichokionyesha kwenye michezo ya fainali za mataifa ya Afrika zilizomalizika hivi karibuni nchini Ivory Coast.
Tanzania inashika nafasi ya 30 Barani Afrika ikiwa imepanda kwa nafasi mbili juu kutoka nafasi ya 32.
Kinara Duniani.
- Argentina
- Ufaransa
- England
Vinara Afrika
Ukanda wa Cecafa