Rais wa Shirikisho la mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) Dkt Suleiman Mahmoud Jabir amesema michuano ya mapinduzi msimu huu itaanza mwishoni mwa mwezi December, 2023, Ili kupisha kalenda ya michuano ya AFCON 2023 itakayoanza January, 2024 nchini Ivory Coast.
Kwa kawaida Mapinduzi huanza mwaka mpya na kufikia tamati January 13, lakini ukitazama January 13 ndiyo tarehe rasmi ya ufunguzi wa michuano ya AFCON ambapo Tanzania pia itashiriki michuano hiyo.
Kwa kuikwepa michuano ya CAF tutaanza Mapinduzi baada ya sikukuu za Christmas, Michuano ya mwaka huu itakuwa ya kipekee sana, kwanza ni maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, pili itakuwa ni majaribio ya matukio ya AFCON 2027 ambayo Tanzania tutaandaaa,
Watu wasipange kukosa klabu kutoka mataifa manne zimethibitisha Kushiriki, yatakuwa na burudani nyingi, na nichukue nafasi hii kuwakarisha wadau wote wasoka waje katika ardhi ya Utalii Zanzibar” .
Suleiman Mahmoud Jabir, Rais wa ZFF.
Tetesi zinadai kuwa huenda mashindano ya msimu huu yakazishuhudia klabu za Kaizer Chiefs na TP Mazembe pamoja na Klabu zingine kubwa Barani Afrika zikishiriki mashindano ya msimu huu.